Kuelekea mchezo wa watani wa jadi, hatimaye Klabu ya Simba imetamka kuwa
kocha wao msaidizi aliyetua klabuni hapo wiki iliyopita anatarajiwa kukaa kwenye benchi Jumamosi ijayo.
Simba inatarajiwa kucheza dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Uhuru jijin i Dar es Salaam ambapo presha imekuwa kubwa hasa kwa mashabiki kutokana na upinzani wa jadi wa timu hizo.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally amesema kocha huyo msaidizi Masoud Djuma aliyetua klabuni hapo kuchukua nafasi ya Jackson Mayanja amepata vibali na atakuwepo katika benchi kwenye mchezo huo.
Abbas amesema kuwa kuna v itu vinakamilishwa kuhusu v ibali vya kazi na anaamini hadi kufikia Jumamosi kocha huyo atakuwa na nafasi ya kukaa kwenye benchi kwa mara ya kwanza kuanza kuitumikia timu hiyo.

0 comments :
Post a Comment