News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday, 25 October 2017

JACKSON MAYANJA: ASEMA YANGA NDIE BINGWA MWAKA HUU!!

Tokeo la picha la kocha mayanja
KOCHA Jackson Mayanja ambaye amejiengua kwenye kikosi cha timu ya Simba kwasababu zisizojulikana, amesema kwamba pamoja na mwenendo wa timu hiyo katika Ligi Kuu bara lakini nafasi ya Yanga kutetea ubingwa ni kubwa kuliko watu wanavyofikiri. Mayanja amesema kuwa kiufundi timu ya Yanga inaimarika kadri siku zinavyosonga mbele hivyo hataona ajabu akiona wametwaa ubingwa kwa mara ya nne mfululizo. “Nisingependa kuzungumzia namna nilivyoondoka Simba kwasababu yale yalikuwa maamuzi yangu binafsi na wala sikushinikizwa na mtu yeyote, lakini kwa mwenendo wa Ligi ninavyoona Yanga inaweza kushangaza watu mwishoni mwa msimu,” alisema Mayanja. “Mimi kama kocha naweka karata yangu ya ubingwa Yanga kwasababu kila siku naona wanabadilika na kuboresha maeneo yenye upungufu,”aliongeza. Mayanja alitangaza kujiuzulu kuifundisha Simba baada ya kuiongoza kwenye mechi sita za mzunguuko wa kwanza wa Ligi na taarifa zilizopo ni kuwa ataelekea kujiunga na timu ya Kagera Sugar.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment