Mwanza. Mashabiki wa timu ya Alliance SC waliwacheka wachezaji wa Dodoma FC kwa kuwaita madingi jambo ambalo lilimkera Kocha Jamhuri Kihwelu “Julio”na kutamka neno nzito.
Alliance ilikuwa mwenyeji wa Dodoma FC katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza uliopigwa Uwanja wa Nyamagana juzi na ambapo Alliance ilishinda bao 1-0.
Julio alisema licha ya wachezaji hao kucheza muda mrefu, lakini wana uwezo mkubwa uwanjani ambapo kama wangekuwa wazee basi wangekuwa kila mechi wanafunga mabao saba.
“Hakuna wazee kwenye timu yangu hawa ni wachezaji ambao wamecheza soka siku nyingi lakini wana uwezo mkubwa wa kucheza mpira kama wangekuwa madingi si tungepigwa saba na Alliance”alisema Julio.
Julio alisema hawa hawa wachezaji wazee wanaowasema ndio watakaipandisha Dodoma FC Ligi Kuu msimu ujao.


0 comments :
Post a Comment