
BIFU kati ya mapacha wanaounda kundi la muziki la P-square, Peter na Paul, limeendelea kushika kasi na kwa sasa limehamia kwa mashabiki wao wanaotumia mitandao ya kijamii.
Mashabiki wengi wa kundi hilo wamemjia juu Peter wakimshutumu kwa kurekodi video inayoonesha akipigana na ndugu yake huyo.
Video hiyo ilianza kuonekana Jumanne ya wiki iliyopita na imewashtua mashabiki wao wanaoamini P-square inaelekea kufa.
Hata hivyo, asilimia 65 ya mashabiki wanaamini Peter hakupaswa kurekodi video hiyo kwani inalimaliza kabisa kundi lao.
Ingawa huenda Peter alikuwa na sababu zake za kurekodi video hiyo ya dakika chache, mashabiki wanaamini alitakiwa kuifanya kuwa siri na si kuwafikia watu wengi
VIDEO HIO HAPO CHINI IONE HAPA!!


0 comments :
Post a Comment