News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 1 October 2017

HII NDIO REKODI KATI YA SIMBA VS STAND UNITED:JAPO HII REKODI KWA GEMU LA LEO TUPA KULE!!

Simba itakuwepo uwanjani leo kukipiga dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage lakini kazi itakuwa ngumu kwa timu zote kutokana na presha.
Simba inacheza leo mechi yake ya tano ya ligi ugenini dhidi ya Stand United, iwapo itashinda itafikisha pointi 11 na kuitoa Mtibwa kwenye uongozi wa ligi kwa sababu ‘Wekundu wa Msimbazi’ wana idadi nzuri ya wastani wa magoli.
Rekodi inaibeba Simba katika mechi ambazo imecheza dhidi ya Stand United, katika michezo sita iliyopita Simba imeshinda mara nne, Stand imeshinda mara mmoja na mchezo mmoja timu hizo zilitoka sare.

REKODI ZA SIMBA Vs STAND UNITED
12/05/2017 Simba 2-1 Stand United
02/11/2016 Stand United 0-1 Simba
13/02/2016 Stand United 1-2 Simba
30/09/2015 Simba 1-0 Stand United
21/02/2015 Stand United 1-0 Simba
04/10/2014 Simba 1-1 Stand United
Hadi sasa kila timu imeshacheza mechi nne za ligi msimu huu, Simba imeshinda michezo miwili na kutoka sare mara mbili wakati Stand United yenyewe imeshinda mechi moja tu katika michezo minne waliyocheza tangu kuanza kwa msimu.

STAND UNITED MSIMU HUU
Mtibwa Sugar 1-0 Stand United
Lipuli 1-0 Stand United
Stand United 0-Singida United
Stand United 2-1 Mbeya City
SIMBA MSIMU HUU
Simba 7-0 Ruvu Shooting
Azam 0-0 Simba
Simba 3-0 Mwadui
Mbao 2-2 Simba
Simba bado haijashinda ugenini msimu huu, imecheza mara mbili nje ya uwanja wa Uhuru na kuambulia sare (Azam 0-0 Simba, Mbao 2-2 Simba). Stand imeshinda mechi moja tu kati ya nne ilizocheza, imeshinda nyumbani (Stand United 2-1 Mbeya City) huku ikiwa imepoteza mechi mbili ilizocheza nje ya Shinyanga (Mtibwa Sugar 1-0 Stand, Lipuli 1-0 Stand).
USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA Millionaire  Ads
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment