Arsenal itawaalika timu mpya iliyopanda daraja kucheza Ligi Kuu nchini Uingereza msimu huu, Brighton kwenye dimba la Emirates.
Arsenal imekuwa na rekodi tamu na ya kusisimua dhidiya tim zinazopanda daraja kwani haijafungwa kwenye michezo yake 31 ya ligi hiyo, wakishinda michezo 26 na kwenda sare kwenye michezo 5. Kwenye michezo hiyo imejikusanyia pointi 83 kutoka kwenye uwezekano wa kukusanya pointi 93 tangu ilipopoteza kwa mara ya mwisho kutoka kwa QPR mabao 2-1 Machi 2012.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa Arsenal na Brighton tangu walipokutana mwaka 1983, lakini wakati huu Arsenal ipo kwenye mbio za kukiwania kilele cha msimamo wa ligi.
Taarifa kutoka kwenye klabu ya Arsenal zinaeleza kwamba, Alexis Sanchez, Lacazette, Aaron Ramsey na Granit Xhaka wote wanarejea baada ya kupumzishwa katikati ya wiki kwenye safari ya Belarus kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Santi Cazorla, Francis Coquelin, Danny Welbeck na Calum Chambers watakuwa nje ya uwanjakutokana na majeraha.


0 comments :
Post a Comment