PSG siku hizi nayo imekuwa klabu gumzo sana duniani, imekuwa klabu ambayo waandishi wengi wanaitolea jicho kutokana na kutopungukiwa na vichwa vya habari na matukio kila kukicha.

Wakati sakata la Neymar na Cavanni likiendelea sasa yameibuka mapya ambapo mshambuliaji wa klabu hiyo Ben Arfa anapanga kuishitaki klabu hiyo kutokana na jinsi wanavyoishi naye huku ana mkataba na klabu hiyo.
Ben Arfa ambaye aliwahi kuichezea Newcastle ya nchini Uingereza ametoswa katika kikosi cha kocha Unai Emery tangu msimu huu wa ligi uanze huku pia klabu hiyo ikizuia jaribio la Arfa la kuihama timu.

Wakili wa Arfa aitwaye Jean Bertrand amesema wameshaiandikia barua PSG juu ya suala hilo huku akisisitiza kwamba klabu hiyo imemkosea sana heshima Arfa kwa kipindi kirefu na sasa wanaona ni vyema kuchukua hatua.
Bertrand amesema klabu hiyo haijawahi kukutana na Arfa bali maagizo yote wanampigia simu tu bila ufafanuzi, kilichomuuma zaidi Arfa na kambi yake ni kitendo cha PSG kumlazimisha afanye mazoezi na wachezaji wa akiba bila sababu maalum.


0 comments :
Post a Comment