Klabu ya Inter Millan inataka kuwanyakua nyota wawili kutoka Manchester City, David Silva na Eliaquim Mangala.
PSG itampa bonasi ya pauni milioni 10 nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez kama atasaini mkataba wa awali mwezi Januari.
Idrissa Gueye amempa motisha meneja Ronald Koeman baada ya kukubali kusaini mkataba wa muda mrefu wa kuendelea kusalia Everton.
Tottenham huenda ikakubali uhamisho wa nyota kutoka Fulham, Ryan Sessegnon lakini bei ya uhamisho huo ni pauni milioni 50.
Bosi wa Everton, Ronald Koeman anataka mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Andy Carroll kurejea Merseyside mwezi Januari kwa dau la uhamisho la pauni milioni 20.
Arsenal imepanga kumuongezea mkaba mpya wa miaka minne kiungo wake, Jack Wilshere.



0 comments :
Post a Comment