News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 1 October 2017

HAYA NDIO MAMBO MAKUBWA MATANO YALIYOJITOKEZA KWENYE MTANANGE WA YANGA VS MTIBWA

Yanga ilikwenda sare ya bila kufungana dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa siku ya Jumamosi jijini Dar es salaam. Wakisafiri kutoka kwenye mashamba ya miwa, Turiani mjini Morogoro, Mtibwa walionesha dhamira ya dhati ya kuhitaji kuendelea kukalia usukani wa ligi hiyo kwani mpango wa pili kwao ulikuwa ni kupata sare kwenye mchezo huo.
Yafuatayo ni mambo matano yaliyojitokeza kwenye mchezo huo.
Vita ya Donald Ngoma na Stamil Mbonde.
Wote walikuwa na miili iliyoshiba, misuli iliyojengeka haswa! Kama ni uchokozi basi Stamil Mbonde atakuwa ndiyo mchokozi, kila alipokuwa Ngoma karibu na lango lao alihakikisha anamghasi na hakumwacha awe huru kuamua alitakalo. Mfano mzuri ni pale ilipotaka kupigwa kona, Stamil alimghasi sana Ngoma kiasi kwamba mshambuliaji huyo akaonekana kukerwa na kuruashiana vijimaneno na Stamil. Hakika walikuwa kwenye vita ya kimchezo.
Ajib akaze kamba za viattu vyake!
Ni wazi kwamba alikuwa kwenye kiwango kizuri, aliipa uhai mkubwa Yanga kwenye safu yake ya ushambuliaji lakini anahitaji kuziangalia vizuri kamba za viatu vyake huenda zikawa zimelegea, alionekana kukosa mabao yaliyokuwa ndani ya uwerzo wake. Alionekana kutokuwa mwiba mkali sana kwa kukosa nguvu ya kupambana na miiliya walinzi wa Mtibwa, kwenye dakika ya 73 Godfrey Mwashiuya aliingiza mpira wa krosi uliomkuta Ajib alipiga shuti lililookolewa na Benedict Tinoko baadae mpira ukamkuta Buswita naye akashindwa kufunga, labda ubora wa Tinoko ulisaidia lakimni Ajib angeweza kufanya zaidi.
Salum Kimbwanda mambo safi.
Kiungo wa mtibwa, Salum Kimbwanda alikuwa na mchezo mzuri licha ya kutolewa kwenye dakika ya 81 na kuingia Henry Joseph Shindika. Alionesha uwezo wa kukimbia na mipira kwa dakika zote naiikuwa si rahisi kumuona akiwa anatembea bila malengo, tatizo kubwa ni kwamba bado hakuwa na uwezo mzuri wa kujua ni eneo lipi sahihi mpira unahitaji kwenda, pia matumizi sahihi ya wakati, hakujua ni wakatiupi atoe pasi na wakati upi apige mipira langoni.
Yondani nyota wa mchezo, Andrew Vincent mmmmh!
Kwenye mchezo wa jana, Kelvin Yondani alifanya kazi nzuri sana kuwazuia washambuliajiwa Mtibwa Sugar,aliondosha mipira yote ya hatari na aliweza kuanzisha mijongeo ya hatari kuelekea katikati mwa uwanja. Hakika alikuwa nyota wa mchezo kama hakuwepo nyota mwingine wa mchezo. Andrew Vincent alifanya kazi nzuri lakini kwenye mashambulizi ya nguvu, hakuweza kuyafanya kwa usahihi ndiyo maana Youthe Rostand alionekana kumfokea na kulalamika baada ya Mtibwa kukaribia kufunga kipindi cha pili.
Gadiel Michael alijitakia kadi ya njano.
Alioneshwa kadi ya njano kwenye dakika ya 68 baada ya kuushika mpira kwa makusudi akidhani umetoka wakati haikuwa hivyo. Hii ni kadi ya kujitakia kwasababu siku zote mchezaji anatakiwa kucheza na filimbi ya mwamuzi.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA Millionaire  Ads
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment