
NAHODHA wa Azam, Himid Mao, amesema hana presha hata kidogo ya kuivaa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayochezwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MWANASPORTS LEO, Himid alisema anaamini kikosi chake ni bora kuliko wapinzani wao, kwani dakika 90 zitaamua matokeo.
Himid alisema hana presha, kwa kuwa anajua matokeo ya mechi hiyo yanaamuliwa uwanjani.
Alisema anaamini kocha wao, Aristica Cioaba, anafanya maandalizi mazuri kutegemeana na mechi inayowakabili na kama wachezaji wenzake watazingatia maelekezo yake ushindi utakuwa wao.
“Sina hofu yoyote ya mechi na si kawaida yangu kuhofia timu, tutacheza na Simba, naamini mwalimu anafanya maandalizi yake kulingana na timu tunayokwenda kukutana nayo,” alisema.
Katika mechi ya kwanza ya ligi hiyo, Azam waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara, wakati Simba waliifunga mabao 7-0 Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*

0 comments :
Post a Comment