HAWA AZAM ????? MBONA WETU HAWA KABISAAA!! TSHABALALA
Dar es Salaam. Beki wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema hawana presha yoyote kuelekea katika mchezo wao ujao dhidi ya Azam utakaofanyika Jumamosi hii.
Simba ilianza mchezo wake wa kwanza wa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuifunga Ruvu Shooting mabao 7-0 huku Azam yenyewe ikipata ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Ndanda.
“Tuko kwenye kiwango kizuri kwa sasa hivyo hatuna wasiwasi wa kupata matokeo ya ushindi,”alisema Tshabalala.
Mchezo huo utachezwa Jumamosi kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Azam Complex.
Beki Mghana amkamia John Bocco Chamazi
BEKI mtata wa Azam, Yakubu Mohammed ameionya Simba kuwa ikijaribu kumtumia straika John Bocco katika mchezo wao wa keshokutwa Jumamosi, wataambulia patupu na kuondoka na aibu.
Yakubu ambaye ameichezea Azam mechi 14 mpaka sasa huku timu hiyo ikiruhusu mabao mawili tu kwenye mechi hizo, ameliambia Mwanaspoti kuwa wanafahamu Bocco hayuko fiti hivyo akipangwa kwenye mchezo huo itakuwa kazi nyepesi kwao kumzuia.
Beki huyo raia wa Ghana alikwenda mbali na kudai hata mshambuliaji Emmanuel Okwi akicheza kwenye mchezo huo hataweza kufua dafu kwani timu yao ya Azam ndiyo yenye beki bora zaidi Ligi Kuu.
“Hata akicheza Okwi (Emmanuel) hawezi kufanya kitu kikubwa, Azam ina beki makini na imara, siyo rahisi kufungika,” alisema Yakubu ambaye anacheza sambamba na Aggrey Morris na Daniel Amoah kwenye nafasi ya ulinzi.
“Wanaweza wakawa wameshinda saba ama tano lakini hiyo siyo sababu ya sisi kuogopa. Wamezifunga timu nyingine na hii ni Azam, timu imara sana,” alifafanua.
“Akicheza Bocco (John) itakuwa kazi nyepesi zaidi. Tunafahamu kwamba ndiyo ameanza mazoezi wiki hii, hatakuwa fiti kucheza dhidi yetu. Akipangwa Simba watakuwa wamejimaliza wenyewe,” alisema.
Katika hatua nyingine, Azam imepanga kumtumia straika wao Yahya Mohammed kuimaliza Simba itakapotua kwenye Uwanja wao wa Azam Complex, kwa mara ya kwanza.
Mohammed ambaye aliomba kutozungumzia mchezo huo, alifichua kwamba rekodi zake kwa sasa zinakwenda poa kwani amefunga mabao manne katika mechi nne za mwisho alizocheza.
Straika huyo aliyekwenda hewani na kushiba, aliifungia Azam bao pekee la ushindi dhidi ya Ndanda kwenye mechi ya ufunguzi wa Ligi huku akifunga mabao mengine matatu katika mechi tatu za kirafiki jambo ambalo limemfanya kuwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 90.
KIPA AZAM FC, AICHIMBA MKWARA SIMBA
KIPA wa Azam FC, Benedict Haule, ameichimba mkwara Simba na kusema kama mwalimu atampanga yeye katika mchezo huo, atawafanyia zaidi ya kile alichokifanya katika mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho (FA).
Akizungumza na BINGWA jana, Haule alisema kocha wao ndiye mwenye uamuzi wa kipa gani ampange siku hiyo na anatamani asimame yeye langoni, ili kuwaonyesha Simba kuwa hakubahatisha pale Dodoma.
“Sina ninachohofia kama kocha atanichagua mimi kudaka katika mechi hiyo sawa, nipo tayari na siwezi nikaogopa kwa sababu wanaounda kikosi cha Simba ni wachezaji kama sisi ukizingatia mechi yangu ya kwanza kubwa nilikutana na timu hiyo,” alisema.
Alifafanua kuwa mchezaji siku zote hatakiwi kuogopa mchezo, hasa anapokutana na timu inayodhaniwa kuwa kubwa, hivyo jambo la msingi ni kuzingatia maelekezo ya mwalimu na kupambana kushinda
Mo aitangazia kiama Azam
Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba, Mohammed Ibrahim ‘Mo Ibra’ amesema sasa wapo tayari kuivaa Azam na kulipiza kisasi cha msimu uliopita.
Simba na Azam zitakutana katika mchezo wa Ligi Kuu Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru, huku Simba ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa kwenye mchezo wa mwisho uliozikutanisha timu hizo.
Ibrahim alisema kwa sasa kikosi cha Simba kina njaa ya mafanikio na itakuwa vigumu kuziacha pointi tatu watakapokutana na Azam.
“Tuna timu nzuri iliyokamilika, kukosa mabao ni sehemu ya mpira. Tunakwenda kujirekebisha kabla ya kucheza na Azam,”alisema Mo ambaye alifunga bao pekee katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Fa iliyozikutanisha timu hizo, Mei mwaka huu.
Jana Jumapili, Simba ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Hardrock ya Pemba na licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 washambuluaji Laudit Mavugo na Juma Liuzio walikosa mabao mengi ya wazi.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja alisema Simba itafanya vizuri kwenye mchezo wa Azam kwakuwa baadhi ya wachezaji wake muhimu watakuwa wamerudi kikosini.
“Wanasimba wawe watulivu, kila mchezaji aliyesajiliwa ana nafasi yake. Niyonzima, Okwi na Juuko tumewakosa leo, lakini ni wachezaji muhimu. Kujiandaa kwetu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo,”alisema Mayanja, akiwatetea washambuliaji wake.
HIMID: SINA PRESHA HATA KIDOGO NA SIMBA
NAHODHA wa Azam, Himid Mao, amesema hana presha hata kidogo ya kuivaa Simba katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayochezwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Himid alisema hana presha, kwa kuwa anajua matokeo ya mechi hiyo yanaamuliwa uwanjani.
Alisema anaamini kocha wao, Aristica Cioaba, anafanya maandalizi mazuri kutegemeana na mechi inayowakabili na kama wachezaji wenzake watazingatia maelekezo yake ushindi utakuwa wao.
“Sina hofu yoyote ya mechi na si kawaida yangu kuhofia timu, tutacheza na Simba, naamini mwalimu anafanya maandalizi yake kulingana na timu tunayokwenda kukutana nayo,” alisema.
Katika mechi ya kwanza ya ligi hiyo, Azam waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara, wakati Simba waliifunga mabao 7-0 Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mkude:Mechi ya Azam inataka akili zaidi
Dar es Salaam. Kiungo mkabaji wa Simba,Jonas Mkude amesema mechi dhidi ya Azam inahitaji akili zaidi.Simba watakuwa wageni wa Azam, Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara.
"Azam si timu ya kubeza walianza vema mechi yao na Ndanda kwa kuwafunga bao 1-0 na kujikusanyia pointi tatu na sisi tuliwafunga Ruvu Shooting kwa mabao 7-0, kila mtu ana hamu ya kuona anaendeleza furaha,"alisema Mkude.
Alisema anaamini Simba itaibuka na ushindi mnono dhidi ya Azam kwa madai wamejipanga kuhakikisha wanaendeleza gurudumu la ushindi.
"Hakuna kazi rahisi kwani kila timu ipo kwa ajili ya kuvuna pointi tatu ndivyo ilivyo na kwetu kuona tunafika mbali na mwisho wetu uwe ubingwa,"alisema Mkude.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*

0 comments :
Post a Comment