
London, England. Winga wa Leicester City, Riyad Mahrez imebainika kuwa lengo lake ilikuwa kujiunga na Manchester United msimu huu.
Mahrez aliondoka katika kambi ya timu yake ya Taifa ya Algeria katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho kwa ajili ya kuvizia uhamisho wa kwenda Manchester United lakini timu hiyo ambayo ilishafanya nae mazungumzo ilimkatia mawasiiano dakika za mwisho hivyo akashindwa kakamilisha dili hilo
Man United ilionyesha dalili za kumtaka staa huyo katika siku za mwisho ikiungana na AS Roma, Barcelona na Arsenal, lakini hakuna timu yoyote kati ya hizo ambayo ilitoa ofa rasmi kwa Leicester City na sasa mchezaji huyo amerudi kambini.

0 comments :
Post a Comment