News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Tuesday, 15 August 2017

YANGA YAMSAINISHA KABAMBA TSHISHIMBI MIAKA 2

Klabu ya Yanga hatimaye imefanikiwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili kiungo kutoka Congo Papy Kabamba Tshishimbi.

 Baada ya kukamilisha taratibu hizo, Tshishimbi (jana) amesaini mkataba wa miaka miwili  mkataba  huo aliusaini  mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika.

Baada ya kusaini mkataba Mcongo huyo  anayesemekana kuwa ndiye mrithi Haruna Niyonzima aliyesajiliwa Simba Sc kwenye Usajili huu anatarajiwa kuondoka  Dar es Salaam leo kwenda kisiwani Pemba kuungana na kikosi cha Yanga kwa maandalizi ya msimu mpya na  mechi ga Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Agosti 23.

Usajili wa Tshishimbi umefikisha wachezaji 6 wa kigeni kati ya 7 wanaotakiwa kwa mjibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara ambao ni kipa
1:Youthe Rostand
2:Thabani Kamusoko
3:Kabamba Tshishimbi.
4:Donald Ngoma
5:Amissi Tambwe
6:Obrey Chirwa.

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment