News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday, 14 August 2017

HAYA NDIO MAJIBU YA MZEE KILOMONI :BAADA YA KUMUULIZA USHATIMULIWA VIPI KUHUSU KESI NA KUHUSU KUJIUNGA NA YANGA?



Siku moja tangu Klabu ya Simba kupitia mkutano wake mkuu itoe tamko kuhusu mzee Hamis Kilomoni kusimamishwa uanachama na kuvuliwa uongozi wa ujumbe wa baraza la wadhamini, mkongwe huyo ameibuka na kujibu mapigo.
Akizungumza juu ya maamuzi hayo ya Simba yaliyofanywa kwenye mkutano mkuu uliofanyika jana kwenye Ukumbi wa Mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam, mzee Kilomoni amesema msimamo wake juu ya kile alichokuwa akikitetea upo vilevile na hajaubadilisha.
Mzee Kilomoni ameongeza kuwa yeye na wenzake ndiyo waasisi wa Simba, hayo maamuzi yaliyofanywa jana hayamtishi na wala yeye hatabadili uamuzi kwa kuwa anaamini kile anachokifanya.
Amesisitiza kuwa keshi aliyofungua itaendelea vilevile lakini kama kutakuwa na sheria zimefuatwa juu ya sakata hilo basi yeye hatakuwa na kipingamizi lakini ka hali ilivyo sasa, hakuna ambacho anaona kimembadilisha pia ameshangaa taarifa za kuhusishwa na Yanga na kusema wao ndio waanzilishi wa Simba kwahio hawezi kuacha chake kwenda kwa vya watu hata siku moja

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment