Ronaldo ambaye alifunga bao moja katika kipute hicho dhidi ya Barcelona, alipewa kadi nyekundu baada ya kujiangusha ndani ya eneo la wapinzani na ndipo mwamuzi akampa kadi ya pili ya njano lakini wakati akilalamika, alimsukuma mgongoni.
Katika mchezo huo ambao Real Madrid walipata ushindi wa mabao 3-1 inaonyesha kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 96 cha kanuni za soka za Chama cha Soka cha Hispania kitendo cha kumsukuma mwamuzi kinaweza kumfanya mchezaji afungiwe mechi nne hadi 12.* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment