Beki wa kati wa Simba, Mganda, Juuko Murshid amerejea nchini Tanzania wiki hii kuungana na wenzake katika maandalizi ya msimu ujao wa 2017/18.
Juuko alikuwa katika mchakato wa kujiunga na Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, lakini imeonekana dili hilo limekwama kutokana na kile kilichoelezwa kwamba ni kutoafikia pande mbili za klabu hizo.
Pichani ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hans Poppe akiwa na beki huyo wa kimataifa Juuko Murshid.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment