Simon Msuva ameendelea kuwa na maisha mazuri nchini Morocco baada ya kufunga bao katika mchezo wake mwingine wa akiwa na Difaa Hassani El-Jadida (DHJ) inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco ‘Botola’.
Winga huyo wa zamani wa Yanga, jana alifunga bao moja katika mechi ambayo timu yake ilipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Union Sportive Musulmane Oujda kwenye Uwanja wa Uwanja wa El Abdi, Jadida.
Msuva ambaye amekuwa mfungaji mzuri tangu alipotua Morocco, alisaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na timu hiyo Julai 28, mwaka huu baada ya kuichezea Yanga tangu mwaka 2012 akitokea Moro United
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment