Licha ya kuwa winga Ramadhani Singano alikuwa akiwania na Yanga ambapo tayari mazungumzo yalikuwa yameshafanyika ili asaini kikosini hapo, mchezaji huyo amepiga kona na kurejea katika timu ya Azam FC.
Singano alimaliza mkataba na Azam FC mwezi uliopita, alisafiri kwenda nchini Morocco kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kujlipwa lakini alishindwa kuafikiana na klabu iliyompeleka kwa kile kilichoelezwa kuwa wakala wake ndiye aliyechangia kuvurugika kwa dili hilo.
Baada ya kurejea jijini Dar es Salaam alikuwa mchezaji huru ambapo ilifahamika kuwa Yanga ilimhitaji na tayari makubaliano yalishafikiwa kilichobaki ni kusaini.
Awali Singano mwenyewe alisema baada ya kurejea nchini alifuatwa na timu tatu kumshawishi asajili ambazo ni Azam FC, Singida United na Yanga.
Akizungumzia usajili huo, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd alisema ni kweli wamemrejesha kundini Singano na ameshasaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo
0 comments :
Post a Comment