News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 6 August 2017

Kauli ya kocha wa Singida United baada ya kuchabangwa 3-2 na Yanga africans


Kocha wa Singida United Hans van Pluijm amesema ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga licha ya kufungwa 3-2 na mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita.
Pluijm amesema wachezaji wake wamecheza kwa nidhamu na kuzingatia yote aliyowaagiza japo kulikuwa na makosa machache ambayo benchi la ufundi watakaa na kuyafanyia kazi.
“Kwa ujumla vijana wamecheza vizuri sana, nimevutiwa na kiwango chao. Hatukuwa tukihitaji sana ushindi bali tulikuwa tunafanya tathmini ya kiufundi na kuona wapi kuna mapungufu kwa ajili ya kufanya marekebisho kabla ya kuanza kwa ligi,” Hans van Pluijm.
“Wamecheza kwa kuzingatia maelekezo tuliyowapa licha ya kupoteza mechi lakini bado nimevutiwa sana kiufundi na hicho ndio kitu muhimu tulichokuwa tunakitaka.”
Kuhusu wachezaji wake kukosa penati, Hans amesema ni kitu cha kawaida japo wapigaji wanatakiwa kuwa wamejiandaa kabla ya kuamua anataka kupiga upande gani.
“Kichwani unatakiwa kuwa unajua unapeleka wapi mpira hivyo ndivyo unavyoweza kufunga penati, sio hapa tu vinatokea duniani kote.”
Magoli ya  Yanga yamefungwa na Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe na Emanuel Martin wakati Singida United wao walifunga kupitia kwa Danny Usengimana na Shafiq Batambuze.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment