News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 6 August 2017

VIDEO:TFF YAWACHINJIA MBALI SHAFII DAUDA NA WENZIE YASEMA NI KWELI YALIYOSEMWA NA TAKUKURU


Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limejiridhisha kuwa wote waliokamatwa na TAKUKURU mkoani Mwanza walikuwa katika kampeni ya uchaguzi na hivyo imewaondoa wagombea hao katika kinyanganyiro hicho.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amefafanua juu ya hilo kwa kusema kulikuwa na kamati ya uchaguzi ambayo kati ya moja ya ajenda zake ilikuwa ni kupitia majibu kutoka TAKUKURU kwa kile kilichotokea Mwanza.
Imebainika kuwa wale waliyokamatwa Mwanza walikuwa katika kampeni na kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria kanuni ya 14 kipengele cha tatu inazuiwa mapema.
Alisema kampeni zitatangazwa tu pale watakapo ruhusiwa na kwa msingi huo adhabu ya kikanuni ni kuwaondoa kwenye kinyang’anyiro ama mchakato lakini bado wanahaki kwa msingi huo wanaweza kukata rufaa.
Baadhi ya wagombea hao, yumo mwana habari Shaffih Dauda ambaye alidai alifanyiwa mchezo mchafu katika tukio hilo na kutangaza kujiondoa. 
                                 ANGALIA VIDEO HAPO CHINI
                       
               
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment