WACHEZAJI STARS WAINGIA KAMBINI, ‘MAPRO’ KUANZA KUWASILI KESHO
KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana, kimeanza mazoezi leo
Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, huku nyota wanaocheza nje wakitarajiwa kuwasili kuanzia kesho.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas ameiambia mwanasports leo kwamba wachezaji wote wanaocheza hapa nchini waliingia kambini jana, huku wanaocheza nje wakitarajiwa kuwasili kuanzia kesho.
“Jana jioni wachezaji wa timu za Azam FC, Yanga pamoja na Simba SC waliingia kambini na kikubwa cha kwanza Daktari wa timu aliwapima afya zao leo asubuhi na jioni timu ikaanza mazoezi Uwanja wa Uhuru, “amesema.
Lucas amesema kwamba msafara wa wachezaji 18 na viongozi tisa kutoka Botswana unatarajiwa kuwasili Alhamisi kabla ya kufanya mazoezi katika Uwanja utakaotumika kawa mechi Ijumaa.
“Wenzetu tumewasiliana nao na wamesema watakuja na wachezaji 18 na viongozi tisa, tunazungumzia msafara wa watu 27 na timu itafika Agosti 31, lakini hatujajua ni muda gani watawasili,”amesema.
Lucas amesema wamekwishafanya mawasiliano na wachezaji wanaocheza nje walioitwa kujiunga na kikosi cha Stars akiwemo Nahodha, Mbwana Ally Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji, Farid Mussa wa CD Tenerife ya Hispania, Simon Msuva wa Difaa Hassan El –Jadida ya Morocco na Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini na wote wanatarajiwa kuanza kuwasili kesho.
Kuhusu suala la Uwanja utakaotumika katika mechi hiyo Alfredy amesema, wamethibitisha Uwanja wa Taifa upo katika ukarabati ulioanza siku tano zilizopita na mchezo dhidi ya Botswana sasa ni rasmi utapingwa Uwanja wa Uhuru.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment