Haji Manara ambaye ni Ofisa Habari wa Simba, ametoa taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusu wachezaji woa waliokuwa majeruhi. Taarifa kamili hii hapa:
Klabu ya Simba inayofuraha,kuwaambia kuwa wachezaji wake John Bocco na Haruna Niyonzima, ambaye alipata majeraha madogo juzi wameshaanza mazoezi na wenzao jana.
Huku pia Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu naye anatarajiwa kuanza mazoezi siku chache zijazo baada ya madaktari kuthibitisha uzima wa afya yake.
Pia Klabu inawaomba washabiki wake kote nchini kuendelea kuiunga mkono timu yao ili iendelee kufanya vizuri kwenye ligi kuu iliyoaanza wikiendi iliyopita* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment