BUSUNGU NASIKITIKA SIJAWAFUNGA "WAHENGA" WALIOUA KIPAJI CHANGU
NA ZAINAB IDDY
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Malimi Busungu ambaye sasa anakipiga katika timu ya Lipuli FC, amesema hajafurahia kitendo cha kushindwa kuifunga timu yake ya zamani.
Baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Yanga ambao ni mabingwa waliamua kuachana na straika huyo waliyemsajili akitokea timu ya Mgambo Shooting ya mkoani Tanga.
Busungu alitoa kauli hiyo jana baada ya mchezo kati ya Yanga na Lipuli uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam juzi kumalizika kwa timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.
“Tumepata matokeo ya sare ambayo yalikuwa ni malengo yetu ndio maana tunashangilia, lakini binafsi sijafurahi kwa kuwa nimeshindwa kuifunga Yanga.
“Lengo langu katika mechi hii lilikuwa ni kuhakikisha ninaifunga Yanga ili kuwaonyesha kwamba bado nina uwezo wa kucheza soka ingawa wao ndio waliosababisha nikapoteza kiwango changu,” alisema Busungu.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment