Brazil imeanza maandalizi ya kujiandaa na mechi yake ya kuwania kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Ecuador.
Kati ya walio katika kikosi hicho ni Philippe Coutinho ambaye hajaanza kuichezea timu yake ya Liverpool msimu huu kwa madai kuwa ana “stresi”.
Lakini ameonekana ni mwenye furaha tu akiwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil akiwa na wenzake kama nahodha, Neymar wa PSG au Jesus wa Manchester City.
Coutinho amekuwa akiweka mgomo baridi kuichezea Liverpool kwa kuwa anataka ahamie Barcelona ambayo imeweka nia ya wazi kutaka kumchukua.
Lakini bado timu hizo mvili hazijafikia mwafaka mambo ambalo linasababisha mchezaji huyo kutoonekana katika kikosi hicho ambacho hats hivyo, kinaendelea kufanya vema.
0 comments :
Post a Comment