Simba ilipata ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, juzi Jumamosi, ndani ya ushindi huo Emmanuel Okwi alitupia wavuni mabao manne.
Baada ya kufunga moja ya mabao yake, Okwi aliuchukua mpira na kuuweka tumboni huku akiwa anashangilia.
Imejulikana kuwa kumbe sababu ya Okwi kufanya hivyo ni kwa kuwa mkewe ni mjamzito.
Imefahamika kuwa baada ya kukabidhiwa mpira wa kutokana na kufunga ‘hat trick’ katika mchezo huo, Okwi alisema mpira huo utakuwa zawadi kwa mke wake kutokana na hali yake aliyonayo ya ujauzito.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment