Tshabalala ambaye alikuwa mapumzikoni akijiuguza mguu, amerudi uwanjani kwa kasi na sasa anataka atakapoanza kuonekana akamilike.
Alipofika hapa Afrika Kusini, akafanya kweli akatoa kiasi cha Rand 3,500 ambazo ni kama laki saba za Kibongo na kununua kiatu hicho.
Tshabalala ataonekana na kiatu hicho ambacho ni Nike ya kupanda kinachoonekana kama kimeungwa na soksi. Amepanga kukivaa katika mchezo wao wa kwanza wa Simba Day na ule wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.
“Kazi yangu mpira, lazima niupe heshima na ndiyo maana hata kununua kiatu hiki sikuona uchungu, ningekuwa msanii ndiyo ningehangaika na mavazi na cheni, lakini mimi ni mchezaji,”alisema
0 comments :
Post a Comment