News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday, 2 August 2017

ALIELTWA KUZIBA PENGO LA NIYONZIMA AIKATAA JEZI YAKE PIA AWAAMBIA WAPENZI WA YANGA WASIMFANANISHE NAE SABABU....



WAKATI mashabiki wa Yanga wakiamini mchezaji wao mpya, Rafael Daudi, ndiye atakayeziba pengo la Haruna Niyonzima, mambo yamekuwa tofauti baada ya kiungo huyo kukataa kuvaa jezi iliyokuwa ikitumiwa na Mnyarwanda huyo.
Rafael juzi alimalizana na mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara akitokea klabu ya Mbeya City, ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh milioni 20 pamoja na ada ya uhamisho Sh milioni 10.
Akizungumza na BINGWA, Rafael alisema ni bora apewe jezi yenye namba nyingine, lakini si namba nane ambayo alikuwa anaitumia Niyonzima.
Alisema akiwa Mbeya City alikuwa akivaa jezi namba tano ambayo katika timu yake mpya ya Yanga inatumiwa na beki mkongwe Kelvin Yondan, hivyo hana uwezo wa kuendelea kuitumia jezi hiyo.
“Mbeya City nilikuwa navaa jezi namba tano, lakini kwa Yanga nitavaa nyingine yoyote, lakini si namba nane kwa kuwa sipendi kufananishwa na mtu mwingine, bali ninataka kucheza kama Rafael.
“Lakini siwezi kuwapangia viongozi kuhusu jezi nitakayovaa, bali itabidi nikubali yoyote, lakini nawaomba mashabiki na wapenzi wa Yanga wasinifananishe na aliyekuwa anaitumia, kwani nimekuja kucheza kama Rafael na nitafanya kile kilichonileta,” alisema.
Katika mazoezi ya Yanga yanayoendelea mkoani Morogoro, kiungo huyo, ambaye bado hajakabidhiwa rasmi jezi atakayoitumia, alivalia jezi namba
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment