News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday, 2 August 2017

BARCELONA WATOA RUHUSA ,WAKALA ASHATANGULIA UFARANSA,JANA AMEWAAGA WACHEZAJI WENZAKE KWENYE UWANJA WA MAZOEZI ALAFU....

Jana kulikuwa na habari kuhusu uhamisho wa Neymar kwenda PSG ambapo alionekana Dubai ikidhaniwa ameenda kukamilisha uhamisho huo, baadaye Neymar alipanda ndege na kurejea mjini Barcelona.
Baada ya kurejea Hispania ikaanza kupunguza tetesi za uhamisho wake kwenda PSG, lakini haikuwa hivyo bali kurejea kwake Hispania ndio kumeibua habari mpya na kuongeza asilimia uhamisho wake kutokea.
Leo asubuhi Neymar aliwasili katika viwanja vya mazoezi vya Barcelona kama kawaida lakini tofauti na matarajio ya wengi Neymar hakufanya mazoezi na wenzake na baada ya muda aliondoka zake.
Baadaye taarifa kutoka klabu ya Barcelona ilisema mchezaji huyo ana ruhusa maalum kutoka kwa daktari ana tatizo kidogo la kiafya na ndio chanzo cha mchezaji huyo kutofanya mazoezi na wenzake.
Lakini baadhi ya watu waliokuwepo katika uwanja wa mazoezi wa Barcelona wanadai Neymar alikuwa akiaga baadhi ya watu na kuwaambia anakwenda nchini Ufaransa kujiunga na klabu ya PSG.
Neymar aliwasili viwanja vya mazoezi saa 8:45 lakini baada ya dakika 45 tu alionekana akitoka kwa kasi na inadaiwa anawahi Paris huku wakala wake Wegner Ribeiro akiwa tayari amewasili mjini humo kukamilisha dili hilo.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment