Kikosi cha Simba kimemaliza kambi ambayo ilikuwa imewekwa kisiwani Unguja, Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga katika Ngao ya Jamii.
Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo timu zote zilikuwa nje ya jiji hilo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo na maandalizi ya msimu wa 2017/18 kwa jumla.
Wachezaji wa Simba wamewasili Dar es Salaam majira ya saa tano wakiwa na benchi la ufundi baada ya timu hiyo kuwa Unguja kwa siku kadhaa.
Timu hiyo ilirejea Dar kwa ndege na kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kisha kuelekea kambini kujiandaa kwa mchezo huo wa Ngao ya Jamii.* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment