News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday, 21 August 2017

BAADA YA WANACHAMA WA SIMBA KUKUBALI MABADILIKO: SASA HIKI NDICHO KINAFUATA

Baada ya wanachama wa Simba kuamua kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa club yao kutoka mfumo wa sasa kwenda mfumo wa hisa, watu wengi inawezekana wanajiuliza ni kitu gani ninachofuata baada ya hapo.
Rais wa Simba anaekaimu nafasi hiyo kwa sasa Salim Abdallah amesema, tayari Simba imekuwa mpya lakini wanahitaji muda kwa ajili ya kuunda timu maalum kwa ajili ya kusimamia mchakato kuhakikisha mwekezaji anapatikana na kuweka kwenye club.
“Kinachofuatia sasa ni kazi ya kamati ya utendaji kuunda timu ya wataam ambao wanaueledi katika mambo ya masoko na hisa ili kusimamia mchakato huu kutangaza tenda kwa ajili ya wanachama kuomba kuja kuwekeza kwenye klabu ya Simba”, Salim Abdallah, Rais wa Simba anaekaimu nafasi hiyo.
“Utaratibu utatangazwa lakini hiyo kamati ndio itahakikisha kwamba inampata mshindi na itamleta mshindi huyo kwenye kamati ya utendaji na sisi tutaitisha mkutano mkuu kwenda kumthibitisha kwamba sasa mchakato umekuwa rasmi na mwekezaji ndio huyu na Simba itaingia rasmi kwenye mfumo huo kwa utekelezaji.”
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment