Shabiki mmoja wa Barcelona, akiwa amevaa kanzu amejitokeza kupinga ugaidi katika Uwanja wa Camp Nou jijini Barcelona.
Barcelona ilikuwa inaivaa Real Betis na kushinda kwa mabao 2-0 na shabiki huyo akiwa na kanzu alikuwa na bango lake linalowataka watu wajitokeze kuupinga ugaidi kwa kuwa hauna dini.
Katika bango hilo pia kulikuwa na ujumbe wa “Barcelona haiogipi”, hii ni baada ya shambulizi la kigaidi lililotokea siku tatu zilizopita katika jiji la Barcelona na kusababisha vifo vya watu 14.
0 comments :
Post a Comment