Straika wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, amesema kuwa endapo atapata nafasi ya kuanza katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Jumatano hii dhidi ya Simba, anataka kuandika rekodi nyingine.
Tambwe amesema kuwa ana hamu kubwa sana ya kuona akizifumania nyavu siku hiyo kwani amemisi kuifunga timu hiyo. Tambwe amekuwa akiifunga Simba mara kwa mara tangu alipojiunga na Yanga msimu wa 2014/15.
Tangu msimu huo, Tambwe amekutana na Simba mara tano na katika mechi hizo, amefanikiwa kuifunga katika mechi tatu mfululizo.
“Namshukuru Mungu hivi sasa nipo fiti na ninaendelea vizuri na maandalizi yangu kuelekea mchezo huo baada ya kupona goti lililokuwa likinisumbua hivi karibuni.
“Ninamshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema na nipo tayari kwa ajili ya mechi ya Jumatano dhidi ya Simba, kwani nimemisi sana kuifunga jambo ambalo linanifanya nijisikie vibaya kila wakati.
“Endapo nitapata nafasi ya kuanza hiyo Jumatano dhidi ya Simba, nitahakikisha napambana vilivyo ili niweze kuzifumania nyavu roho yangu itulie kwani nataka nizidi kuandika rekodi ya kuifunga mara nyingi,” alisema Tambwe.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment