News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 20 August 2017

PATÀ UCHAMBUZI WA MECHI YA KUKATA NA SHOKA KATI YA CHELSEA VS TOTTEN HAM PATA DONDOO ZOTE ZINAZOWAHUSU HAPA!!@


Uwanja wa Wembley sio uwanja rafiki kwa Tottenham na ni kati ya viwanja mashabiki wa Tottenham hawavipendi lakini leo wanataka kuvunja mwiko na kuondoa laana katika uwanja huo, ikumbukwe huu ni mchezo wa kwanza wa Epl kupigwa katika dimba la Wembley.

Tottenham wanakutana na Chelsea ambao kwa misimu miwili mfululizo wamekuwa wakiwafunga katika michezo muhimu, msimu wa mwaka juzi Chelsea walizima ndoto za ubingwa za Tot na wakafanya tena msimu uliopita, Chelsea wamefungwa mara 2 tu na Tot katika mechi 17 zilizopita.

Tottenham wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu za kufungwa na Chelsea katika michezo muhimu lakini leo Tottenham wanaingia na matumaini kwani kikosi cha Chelsea kinaonekana hakijakaa vizuri.
Chelsea wanaingia katika mchezo huu huku Cesc Fabregas,Garry Cahil,Pedro,Eden Hazard na Diego Costa wakiwa hawapo kwa matatizo mbali mbali ikiwemo adhabu na majeraha na hii inaweza kuwapa nafasi kubwa Tot kuifunga Chelsea.
Tottenham mshambuliaji wao Heung Mi Son anaweza kurejea leo baada ya majeraha yake kuanza kupona huku Danny Rose akiwa kwenye hati hati kukosa mchezo huu kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu.

Chelsea wanaweza kuzidi kupoteana hii leo na kipigo kutoka kwa Tottenham kinaweza kuanza kuchafua hali ya hewa katika klabu ya Chelsea ambapo tayari wachambuzi mbalimbali wameanza kutoa nafasi kwa Antonio Conte kuwa kocha wa kwanza kutimuliwa EPL msimu huu.* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment