BEKI WA YANGA AIVUJISHIA SIRI SIMBA
NA WINFRIDA MTOI
BEKI wa zamani wa Yanga, Stephano Mwasyika, amesema siri ya kushinda mechi ya watani wa jadi ni wachezaji kujiamini na si kuwa na kikosi kizuri.
Mwasyika, ambaye kwa sasa ni nahodha wa timu ya KMC, alisema siku zote mechi za watani hao wa jadi zinakuwa na mambo mengi na mpira hauchezwi kama inavyotakiwa.
Alisema mara nyingi kila timu inaingia uwanjani ikiwa imekamia mechi na kutaka ushindi, huku mpira unaochezwa unakuwa tofauti na michezo mingine ya kawaida.
“Kwa uozoefu wangu kwa mechi za Simba na Yanga, mara nyingi wale wanaosema wana kikosi kizuri ndio wanafungwa, kwa sababu mpira unaochezwa pale si wa kawaida, kinachotakiwa ni ushindi na inategemea na wachezaji walivyoamka siku hiyo,” alisema.
Alisema moja ya vitu vinavyowachanganya ni wingi wa mashabiki wanaofika uwanjani kushangilia, endapo mchezaji hatajiamini hata kama alikuwa anadaiwa mzuri lazima ataboronga
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment