Taarifa ikufikie kuwa kiungo wa Simba, Said Hamisi Ndemla anatarajiwa kuondoka nchini wiki ijayo kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweden.
Awali kiungo huyo aliondoka nchini wiki chache zilizopita kwa lengo hilo hilo lakini alirejea baadaye kukiwa hakuna taarifa rasmi za majaribio yake hayo.
Mtu wa karibu wa Ndemla amesema kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kwenda kufanya majaribioo katika timu ya AFC.
“Visa yake mchezaji huyo ilichelewa kidogo kutokana na taratibu za ubalozi lakini kwa sasa uhakika wa kupatikana Jumanne hivyo kuanzia siku yoyote anaweza kwenye kufanya majaribio,” alisema mtu wa karibu wa mchezaji huyo.
Iwapo Ndemla akifuzu katika majaribio hayo na kuuzwa kwenye klabu hiyo, atakuwa mchezaji ni wa pili kuondoka katika klabu ya Simba kwa sasa baada ya hivi karibuni beki wa timu hiyo, Abdi Banda alitimkia Afrika Kusini kwenye klabu ya Baroka FC inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment