Baada ya Simba kuifunga Gulioni FC mabao 5-0, kumekuwa na maneno mengi juu ya kichapo hicho.
Mashabiki wa Yanga ambao ni wapinzani wakubwa wa Simba wamekuwa wakibedha kuwa Simba imeifunga timu ya daraja la chini na hivyo haina haja ya kujidai kuwa imepata ushindi dhidi ya timu imara.
Sasa kupitia ukurasa wake wa instagram Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amejibu utani huo kwa kuandika haya:
“Gongowazi wanabeza Gulioni wapo daraja la ngapi kisa tumewafunga Tano!hovyooo kama halua za kimbwinde,,waulize wao tulivyowapiga Tano walikuwa daraja la ngapi?Shubamitttt 😂😂”
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment