Timu ya Yanga ilishuka uwanjani kwa mara nyingine leo Jumapili kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Zanzibar kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Katika mchezo huo ambao Yanga ilichezesha vikosi viwili kwa kila kipindi, imepata ushindi wa bao 1-0 huku kiungo wake mkabaji Papi Tshishimbi akiichezea Yanga kwa mara ya kwanza tangu atue nchini juzi.
Tshishimbi alicheza katika dakika 45 za kipindi cha pili katika mchezo huo ambao Yanga ilipata bao lake kupitia kwa beki wa pembeni Haji Mwinyi.
Mwinyi alifunga bao hilo kipindi cha kwanza cha mchezo huo. Yanga ambayo imeweka kambi Pemba kwa wiki sasa, inajiandaa kucheza dhidi ya Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Jumatano ijayo.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment