News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Tuesday 22 August 2017

NINI DIEGO COSTA: HII HAPA LISTI YA WALIOGOMA HADI KUUZWA WENGINE WALIPIGA MKWARA WATAJIFUNGA MAKUSUDI WASIPOUZWA

Tokeo la picha la Diego Costa
straika wa Chelsea, Diego Costa, aliweka wazi mpango wake wa kubaki kwao Brazil hadi mkataba wake na klabu hiyo utakapomalizika, hata kama atakuwa halipwi chochote na mabosi zake hao.
Nyota huyo hana mawasiliano mazuri na kocha wake, Antonio Conte na amekuwa akivumishwa kurejea La Liga katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid.
Hata hivyo, katika historia ya soka, Costa si mchezaji pekee kugomea timu yake akilazimisha kuuzwa.
Dimitri Payet (West Ham)
Payet alikataa kuichezea West Ham mwanzoni kabisa mwa mwaka huu, akishinikiza uhamisho wake wa kwenda Marseille ya Ufaransa. Alisema hataingia uwanjani kuchezea timu hiyo ambayo ilikuwa kwenye vita ya kujinasua kushuka daraja.
Wamiliki wa klabu hiyo, David Sullivan na David Gold, walifanya juhudi kubwa kumshawishi kubaki lakini mwishowe walimkubalia kwenda Marseille kwa pauni milioni 25.
Raheem Sterling (Liverpool)
Manchester City walipeleka ofa mbili Anfield lakini mabosi wa Liver wakaweka ngumu. Walianza na pauni milioni 30 ikashindikana, kabla ya kuweka mezani pauni milioni 40.
Sterling alitamani uhamisho huo lakini Liver wakawa wanachomoa. Akaanza kwa kusingizia anaumwa, hivyo asingeweza kuwa sehemu ya kikosi kilichokwenda barani Asia kwa ajili ya mechi za ‘pre-season’. Hiyo ilikuwa mwaka 2015, kipindi ambacho alikuwa akiwaniwa na Manchester City.
Uongozi wa Liver ulijaribu kumshawishi kusaini mkataba mpya lakini Mwingereza huyo alishikilia msimamo wake wa kuondoka na mwishowe akatua Etihad kwa pauni milioni 49.
Carlos Tevez (Manchester City)
Septemba 2011, Tevez aligoma kuingia uwanjani akitokea ‘sub’ katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.
Kitendo hicho kilisababisha alimwe faini ya pauni 500,000 na ndipo alipoweka mgomo akitaka kuondoka. Kilichofuata ni kurudi kwao Argentina.
Baada ya mvutano wa muda mrefu, mabosi wake wa Man United hawakuwa na njia nyingine zaidi ya kumruhusu kujiunga na Man City. Mabao yake manne katika mechi za mwishoni mwa ligi ziliiwezesha Man City kuipiku Man United na kubeba ubingwa kwa tofauti ya mabao.
Dimitar Berbatov (Tottenham)
Berbatov aliwahi kuisumbua Tottenham kabla ya kuhamia Man United. Kama ilivyokuwa kwa Tevez, Berbatov alikataa kutokea benchi katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle.
Zikiwa zimebaki saa kadhaa kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, ndipo bosi wa Tottenham, Daniel Levy, alipozungumza na Man United na mchezaji huyo kuondoka kwa pauni milioni 30.75. Akiwa Old Trafford, aliweza kushinda vikombe viwili vya Ligi Kuu England.
William Gallas (Chelsea)
Costa anakuwa mchezaji mwingine kuwahi kuisumbua akitaka kufunguliwa mlango wa kutokea. Gallas aliwahi kufanya hivyo mwaka 2006. Mfaransa huyo aligoma kucheza mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA na kisha kukataa kwenda Marekani kwa ajili ya ‘pre-season’.
Cha kuchekesha kuhusu sakata la Gallas na Chelsea ni kwamba, alitishia kujifunga katika moja ya mechi ambazo angekuwa uwanjani.
Mkwara huo mzito uliwashtua mabosi wake wa Stamford Bridge na ndipo walipotangaza kuwa wamemruhusu kwenda Arsenal. Gallas alisaini mkataba wa miaka minne na kukabidhiwa jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na ‘fundi’ Dennis Bergkamp.
Ilimchukua wiki mbili tu kabla ya Gallas kufunga bao lake la kwanza akiwa na uzi wa Gunners. Mchezo huo ulikuwa dhidi ya Sheffield United uliochezwa Septemba 23, 2006. * USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment