News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Tuesday 22 August 2017

MARCO ANSESIO KIMEO CHA BARCELONA KILICHOGEUKA LULU REAL MADRID NA KUWAFUNGA KILA WAKIKUTANA!!

Tokeo la picha la Asensio

CATALUNYA, Hispania

JINA la nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 lilizidi kupaa kwenye ulimwengu wa soka, baada ya mabao yake mawili katika michezo wa El Classico kati ya timu yake ya Real Madrid na Barcelona.
Alianza kuitungua Barca katika mchezo wa kwanza wa Spanish Super Cup uliochezwa kwenye Uwanja wa Camp Nou. Akafanya hivyo tena Jumatano ya wiki iliyopita pale Santiago Bernabeu.
Hata hivyo, kumwona Asensio akiendelea kujenga utawala wake kwenye kikosi cha Madrid, ni pigo kubwa kwa Barcelona kwani walikuwa na nafasi ya kumsajili misimu kadhaa iliyopita lakini ni kama walimwona hajaiva.
Ni miaka mitatu tu iliyopita ambapo Barca wangetumia kitita cha pauni milioni 4 tu kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Hispania.
Mwaka 2014, Mkurugenzi wa soka wa Barca, Andoni Zubizarreta, alianza kukiona kipaji cha Asensio wakati huo mchezaji huyo alikuwa akiichezea Mallorca.
Zubizarreta alivutiwa na uwezo wa Asensio hasa makali yake pindi anapokuwa na mpira katika mguu wake wa kushoto. Licha ya bosi huyo kumpigia debe staa huyo, viongozi wake wa Barca walipuuzia.
Kipaji cha Asensio ambaye kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 17, kilimvutia pia aliyekuwa kocha wa Barca kwa kipindi hicho, Pep Guardiola.
Kuna kipindi ilivumishwa kuwa kinda huyo alikuwa akisaka nyumba mjini Castelldefels, nje kidogo ya Barcelona, ambako mastaa wengi wa klabu hiyo wanaishi.
Lakini, dili hilo halikufanikiwa na mwishowe Asensio alihamia Madrid kwa ada ndogo tu ya pauni milioni 4.
Kumbe, wakati Barca wakivutana ni jicho la aliyekuwa kocha wa Madrid kwa kipindi hicho, Carlo Ancelotti, lilishamwona mchezaji huyo.
Alipotua Madrid alishindwa kukabiliana na ushindani wa namba kikosini na ndipo katika msimu wa 2015-16, alipopelekwa Espanyol kwa mkopo.
Aliweza kufufua makali yake akiwa katika kikosi hicho na aliporudi Madrid, alifunga bao kali katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Sevilla.
Kiwango kizuri alichokionyesha katika mtanange huo ulifungua ukurasa mpya wa maisha yake ya soka, kwani kilimpa nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania.
Licha ya kutokea benchi katika mechi nyingi msimu uliopita akiwa na Madrid, Asensio aliweza kupachika mabao 10.
Mashabiki wa Madrid watamkumbuka zaidi kwa bao lake katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus na lile la ushindi walipokutana na Bayern Munich katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Nyota huyo aling’ara pia kwenye michuano ya mwaka huu ya Euro akiwa na timu ya Taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 21 iliyofanyika nchini Poland.
Katika mechi yake ya kwanza, aliipachikia ‘hat trick’ timu yake ya Hispania katika mchezo dhidi ya Macedonia.
Kwa sasa, mashabiki wa Madrid wanamtegemea chipukizi huyo kuwapa faraja hasa baada ya staa wao, Cristiano Ronaldo, kuwa nje akitumikia adhabu ya kukosa mechi tano.
Kwa kile alichokionyesha Asensio katika michezo miwili dhidi ya Barca, Madrid haionekani kuwa na pengo kubwa licha ya kumkosa Ronaldo kikosini.
Wachambuzi wa soka wanaamini kuwa endapo Mhispania huyo ataendeleza makali yake kwa misimu miwili mfululizo, atakuwa na nafasi nzuri ya kuwa mchezaji tegemeo Bernabeu.
Lakini pia, huenda akaingia kwenye historia ya wachezaji waliowahi kuchukua tuzo ya Ballon d’Or. Kutokana na ubora wa Madrid, haitashangaza kumwona akiiweka mkononi mapema tuzo hiyo kuliko Neymar aliyekwenda PSG.
Huku Asensio akiwa faida kubwa kwa Madrid kwa sasa, Barca waliompuuzia miaka mitatu iliyopita wanahaha kuipata huduma ya Philippe Coutinho ambaye hata hivyo atawagharimu kiasi kisichopungua 100.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment