UBISHI HELA SASA HIVI: MASAU BWIRE NA HAJI MARARA WAWEKEANA DAU LA MAMILIONI SIMBA ASIPOMFUNGA RUVU SHOOTING
OFISA Habari wa klabu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani, Masau Bwire, amesema anasubiri manoti aliyoahidiwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari wa timu ya Simba, Haji Manara, kwani anaamini kikosi chake hakitaweza kufungwa bao 5-0 na Wekundu hao wa Msimbazi.
Haji alitoa kauli hiyo kutokana na aina ya kikosi alichonacho msimu huu, huku akiamini hakuna wa kuwazui katika harakati za kusaka ubingwa.
“Naahidi kumpa milioni tano Masau akaongeze simu nyingine, iwapo tutashindwa kuwafunga Ruvu Shooting mabao chini ya matano,” alisema Manara.
Masau kwa upande wake alisema kuwa, anasubiri kuzipokea fedha hizo kwani anaamini kuwa Wekundu hao wa Msimbazi hawana uwezo huo wa kuwafunga mabao hayo.
“Hawana uwezo wa kutufunga mabao hayo, mimi hivi sasa nasubiri hizo fedha zake tu,” alisema.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment