Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana kesho Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuukaribisha msimu wa 2017/18.
Kuonyesha mchezo huo ulivyo na umuhimu mkubwa, timu zote zilikuwa nje ya Dar kujiandaa, Simba walikuwa Unguja lakini tayari wamerejea tangu jana.
Sasa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea Dar leo saa nane mchana kisha kitaenda kambini kusubiri mchezo huo.
Simba wao walitua Dar kwa ndege wakitokea Unguja wakati Yanga wao wapo Pemba ambapo walikuwa wakijifua kwa nguvu kujiandaa kwa mchezo huo.
Tena amesema kuwa wachezaji watatu ndiyo wataukosa mchezo huo kwa kuwa ni majeruhi ambao ni Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya na Beno Kakolanya, wengine wote waliopo kambini wapo fiti.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment