KAPTEN HAROUB "CANNAVARO" KAKA GK SASA LIPULI TUTAWARIBISHA NA NINI ZAIDI YA KIPIGO CHA MBWA MWIZI??
NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amesema watahakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Lipuli, utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MWANASORTS LEO kwa simu jana, Cannavaro alisema kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, amefanyia kazi upungufu na makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, uliochezwa Jumatano hivyo anaamini watakuwa na ufiti wa kutosha.
Alisema kikosi chao kipo imara, hivyo wana kila sababu ya kushinda katika mchezo huo ili waweze kujitengenezea mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.
“Tuna kila sababu ya kushinda hakuna wa kutuzuia, timu yetu ipo vizuri na kila mchezaji amejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri mechi yetu ya kwanza kwenye ligi, ili tupate pointi tatu ambazo zitatutengenezea mazingira mazuri kwenye msimamo,” alisema Cannavaro.
Cannavaro alisema hawana wasiwasi wowote kwenye mechi hiyo, hivyo hawawezi kuumiza vichwa kwa sababu wapo imara na wana ufiti wa kutosha kwenye kikosi chao.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment