News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 27 August 2017

MKE WA NIYONZIMA ANAELEZA UKWELI WAKE JE ALIKUBALIANA NA MUMEWE KUAMIA SIMBA NA JE FAMILIA IMERIDHIA SWALA HILO ?

niyonzima
MKE wa Mnyarwanda, Haruna Niyonzima anayeitwa, Naillah Uwineza, ameshindwa kuvumilia na kutamka kuwa anaamini kweli mume wake ana Mungu.
Amesema awali alikuwa na hofu kwamba huenda mambo yangemwendea vibaya baada ya mumewe kuhamia Simba kutoka Yanga lakini kumbe sivyo.
Wakati mkewe huyo akisema hivyo, Niyonzima mwenyewe amefafanua sababu ya kwenda kusalimia benchi la ufundi la Yanga siku ya mechi ya Ngao ya Jamii, kuwa ni ujirani mwema tu kwani hajagombana nao.
Naillah ambaye baada ya mchezo wa Simba na Yanga ambao Wekundu wa Msimbazi walishinda kwa penalti 5-4, alikwenda hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kumpongeza mumewe kwa busu motomoto.
“Kwa kweli naamini maombi yanasaidia, presha ilikuwa kubwa na sikuamini kama Haruna angecheza kwa kiwango kile, hakika Mungu ni mkubwa,” alisema.
Kabla ya mchezo huo kuanza, Niyonzima alikwenda kwenye benchi la Yanga na kusalimia wote.
“Nilifanya hivyo kwa sababu mchezo ni amani. Watu wasifikiri kuhama kwenda sehemu nyingine basi mnakuwa maadui si kweli,” alisema.
“Inabidi wakubaliane na mabadiliko kwa sababu mpira ni kazi.”
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment