News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 27 August 2017

KOCHA EVERTON: HAKI YA NANI HILI GOLI LA SIGURDSSON UNAWEZA UKALIA UGALI UKASHIBA " ANGALIA VIDEO YAKE"




Tokeo la picha la Sigurdsson EVERTON EUROPA GOAL
KOCHA wa Everton, Ronald Koeman, ameonekana kupagawa kwa bao lililofungwa na staa wake, Gylfi Sigurdsson, katika mchezo wa kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Europa ugenini dhidi ya Hajduk Split uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Everton ilikuwa ikitafuta matokeo mengine mazuri ya kulinda ushindi wao wa bao 2-0 nyumbani Goodison Park, lakini kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa pili kiliwashtua mashabiki wa timu hiyo kufuatia bao kali la umbali wa yadi 30 lililopachikwa na Josip Radosevic.
Hata hivyo, mashabiki wa upande wa pili na hata wale wa Everton, walibaki midomo wazi kufuatia Sigurdsson kuachia shuti la mkunjo kutoka nusu ya upande wao hadi kwenye nyavu za Hajduk.
“Nililiona lile bao la Sigurdsson ila sidhani kama wote niliokuwa nao kwenye benchi waliliona. Lilikuwa bonge la bao aisee,” alisema Koeman.

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment