News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Friday, 25 August 2017

BABA YAKE MESSI AKUTANA NA MAN CITY KUZUNGUMZIA USAJILI WA MWANAE KUKIPIGA MAN CITY



BARCELONA  
 HISPANIAHALI ni tete pale Barcelona. Hawapumui vizuri kwa sasa. Neymar ameondoka, Philippe Coutinho amezuiwa kuja. Sasa imeibuka habari nyingine mbaya kwa mashabiki wa Barcelona na mabosi wao. Manchester City imemkomalia Lionel Messi.
Inadaiwa Baba wa Messi, Jorge Messi amekutana na Mkurugenzi wa Ufundi wa City, Txiki Begiristain, kuangalia uwezekano wa mwanae kwenda kukipiga City ili kuungana na Kocha Pep Guardiola mwishoni mwa msimu huu.
Messi na baba yake, Jorge wana uhusiano mzuri na Begiristain, ambaye alikuwa miongoni mwa watendaji wa Barcelona mpaka kufikia mwaka 2012 na walikuwa wanaangalia uwezekano wa staa huyo kujiunga na City kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.
Mkataba wa Messi na Barcelona unatazamiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na staa huyo mzaliwa wa Rosario, Argentina yupo huru kuzungumza na klabu zinazomtaka kuanzia Januari Mosi mwakani.
Awali, ilidaiwa Messi alikubali kusaini mkataba mpya hadi mwaka 2021, lakini mpaka sasa hajasaini mkataba huo na kumekuwa na ushauri mwingi juu yake akitakiwa kufuata nyayo za Neymar kuondoka klabuni hapo.
Barca wanadaiwa wana uhakika Messi atasaini mkataba mpya pindi Barcelona watakapofanikiwa kumletea mbadala wa Neymar aliyeondoka ghafla, lakini mpaka sasa wababe hao wa Nou Camp wamekuwa wakihaha bila ya mafanikio.
Inaeleweka kuwa Guardiola amekuwa akitamani kuungana na Messi tena katika kikosi cha City baada ya kupata mafanikio makubwa na staa huyo walipokuwa pamoja Nou Camp ambapo, walifanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ulaya pamoja.
Man City ndio klabu pekee ambayo inaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya Messi baada ya PSG kuamua kumchukua Neymar, lakini vile vile uhusiano kati ya watu wa Man City na Messi ni mkubwa zaidi kutokana na kuwepo kwa watu watatu klabuni hapo ambao, Messi aliwahi kufanya nao kazi Nou Camp. Mwingine aliyepo City na aliwahi kufanya kazi na Messi Barcelona ni Ferran Soriano, ambaye kwa sasa ndiye Mtendaji Mkuu wa City na yeye pamoja na Begiristain ndio waliofanya kazi kubwa kuhakikisha Guardiola anatua City Julai mwaka jana.
Mabosi wa City wapo tayari kumfanya Messi kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani endapo atakubali kutua klabuni hapo, na kuna uwezekano akalipwa vizuri zaidi ya inavyotazamiwa kwa sababu City watampata bure bila ya kulipa kiasi chochote cha pesa.
Wakati huo huo, aliyekuwa mgombea wa urais wa zamani wa Barcelona, Agusti Benedito amedai suala la Messi linatisha zaidi kuliko la Neymar kwani, Messi atakuwa huru tofauti na ilivyokuwa kwa Neymar.
“Bado hajasaini, ni kitu kinachotia wasiwasi. Kesi ya Messi inaweza kuwa mbaya zaidi kuliko kesi ya Neymara kwa sababu mpaka sasa hadi kufikia Januari 1 atakuwa mchezaji huru,” alisema Benedito alipozungumza na kituo kimoja cha redio nchini Hispania.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment