London, England. Siku chake baada ya mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney kutangaza kustaafu kuichezea timu ya Taifa ya England, kocha Gareth Southgate amesema mchezaji huyo ataandaliwa mechi ya mwisho kwenye Uwanja wa Wimbley kwa ajili ya kumuaga.
Kocha huyo aliwasisitiza wachezaji chipukizi kwamba huu ndio muda wao wa kuonyesha makali baada ya Rooney kuwaachia nafasi.
Hivyo uamuzi wa Southgate kumuandalia sherehe ya kumuaga mchezaji huyo ni kutokana na kutambua mchango wake kwa kipindi chote alichoisaidia timu hiyo ya Taifa kwenye mashindano mbalimbali.
0 comments :
Post a Comment