News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday, 27 July 2017

UNAIJUA SIKU NGUMU NA NDEFU AMBAYO MASHABIKI WA ARSENAL WANATAKA IPITE WAJUE MOJA MAANA INAWAPA PRESHA?

Tokeo la picha la arsenal fan crying
HATIMAYE
staa anayewaweka roho juu mashabiki wa Arsenal, Alexis Sanchez, Jumatatu atakutana ana kwa ana na kocha wake, Arsene Wenger, kuzungumzia hatima yake klabuni hapo.
Ukweli ni kwamba hakuna hata mshabiki mmoja wa kweli wa Arsenal anaetaka Sanchez aondoke
Taarifa zimesema mazungumzo yao ndiyo yatakayoibuka na jibu kuwa mchezaji huyo ataongeza mkataba wa mwaka mmoja au ataondoka zake.
Kwa sasa Sanchez anaitumbua likizo nchini kwao Chile ikiwa ni baada ya kuongezwa muda wa mapumziko na Arsenal, kutokana na uchovu wa michuano ya Kombe la Mabara iliyomalizika wiki chache zilizopita.
Mtandao wa Telegraph umedai kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, anatarajiwa kurejea England mapema wikiendi hii.
Wenger ameendelea kusisitiza kwamba, Sanchez hauzwi na hata mwanasoka huyo hajawasilisha ombi lake la kutaka kuondoka Emirates licha ya tetesi zilizozagaa kuwa atatimkia Manchester City au PSG.
“Uamuzi umeshapitishwa na tutakomaa nao. Uamuzi uliopo ni kutouza,” alisema Wenger, kauli ambayo iliungwa mkono na mkongwe David Seaman aliyesema: “Ningefanya lolote kumbakiza kwa sababu ni mchezaji bora mbaye usingependa kumwona akiondoka klabuni hasa kwenda kwa wapinzani wako.”
Gazeti la El Mercurio la Chile limedai kuwa, Man City wanamtaka kwa udi na uvumba fowadi huyo na wamemweka kileleni kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na kocha Pep Guardiola katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.
Endapo Wenger atashindwa kumshawishi Sanchez kubaki hiyo Jumatatu, Man City wana nafasi kubwa ya kumchukua kwani wameweka mezani kitita cha Pauni milioni 50 huku PSG wakiwa na Pauni milioni 44.
Kwa upande mwingine, mashabiki wa Etihad wanaamini kuwa ukaribu wa Sanchez na Guardiola walipokuwa Barcelona, unaweza kuwa silaha nzuri ya kumnasa mpachikaji mabao huyo
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment