HABARI MPYA YA MOTO JIONI HII:YANGA WAMKOSHA MANULA
KIPA wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Aishi Manula, ameelezea kukoshwa na kitendo cha klabu ya soka ya Yanga
kumsajili golikipa chipukizi, Ramadhani Kabwili na kukiri kuwa wamepata jembe.
Kabwili ambaye ni kipa wa timu ya soka ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka mitano.
Akizungumza na TANZANIA HOT NEWS juzi, Manula alisema anamfahamu vizuri kipa huyo baada ya kuwa pamoja katika kikosi cha Azam FC kwa miaka kadhaa.
Alisema uwezo wake ulionekana akiwa katika kikosi cha Serengeti Boys kilichoshirki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana, zilizofanyika nchini Gabon mwaka huu.
Manula aliongeza kuwa kutokana na ubora wake, hata Kocha Mkuu wa Stars, Salum Mayanga, hakuwa na shaka kumwita kikosini baada ya Beno Kakolanya kuumia.
“Kabwili ni kipa mzuri na kila mmoja ameshuhudia uwezo wake, pia ni kijana mwenye hamu ya kupata mafanikio. Serengeti Boys haikufanikiwa kushiriki michuano ya Kombe la Dunia lakini juhudi zake zilionekana,” alisema Manula.
Pia Manula alimshauri Kabwili kuendelea kukaza buti na kupiga hatua zaidi ya alipofikia ili aweze kutimiza malengo yake akiwa ni miongoni mwa vijana ambao Taifa limewekeza kwa kuwaweka kambini kwa muda mrefu wakinolewa
0 comments :
Post a Comment