News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday 27 July 2017

DAAH!! MSIKILIZE ADEBAYOR ALIPOULIZWA JE UCHAWI WA MAMA YAKE NDIO CHANZO CHA KUPOROMOKA? jibu lake litakushangaza...


EMMANUEL Adebayor alipoondoka Arsenal mwaka 2010, alikuwa amefunga mabao 46 katika mechi 104 pekee. Alipokwenda Manchester City akapasia nyavu mara 15 katika michezo 34.
Hata hivyo, makali yake hayakuwa ya muda mrefu kwani msimu wake wa mwisho kuwa kwenye ubora wake ulikuwa wa 2013-14 ambapo alifunga mabao 13 na kutoa ‘asisti’ nne akiwa na kikosi cha Tottenham.
Kipindi hicho, Spurs ilikuwa chini ya kocha mwenye heshima kubwa Ligi Kuu England, Harry Redknapp na Adebayor alijiunga na timu hiyo akitokea Man City.
Ikumbukwe kuwa Man City walianza kwa kumpeleka kwa mkopo Real Madrid lakini aliyekuwa kocha wa mabingwa hao wa La Liga, Jose Mourinho, hakutaka kumnunua moja kwa moja baada ya kumtumia kwa miezi sita pekee.
Katika msimu wa 2015-16, alijiunga na Crystal Palace lakini alishindwa kung’ara kabla ya kutua Basaksheir ya mjini Instanbul, Uturuki, ambayo ndiyo anayoichezea sasa.
Licha ya kuzichezea klabu hizo kubwa, bado mashabiki wake wanaamini staa huyo mwenye umri wa miaka 33, ni kipaji kilichopotea ghafla kwenye ulimwengu wa mchezo huo.
Hata hivyo, nyuma ya pazia inaelezwa kuwa ‘kufulia’ kwa Adebayor kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na mgogoro wake na familia yake akiwamo mama mzazi.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), Adebayor alikiri kuwa familia yake ilichangia kufeli kwake katika kikosi cha Madrid.
“Nilifanya kila kitu kuhakikisha nabaki Madrid lakini marehemu kaka yangu alisababisha niondoke.
“Alituma barua ya familia iliyokuwa ikiwataka Madrid kuniacha. Sisemi ilikuwa sababu ya mimi kuondoka, lakini ilichangia kwa kiasi kikubwa. Hata kama ni kwa asilimia 10 ilichangia sana.
Adebayor aliyewahi pia kuzichezea Metz na Monaco, amedai kuwa bado hana uhusiano mzuri na ndugu zake na wamekuwa hawamtembelei anapokuwa majeruhi ila hufanya hivyo wanapokuwa na shida ya fedha.
Huenda wengi wanajiuliza chanzo cha Adebayor kuchukiwa na ndugu zake. Inadaiwa kuwa mama yake mzazi hafurahii maisha ya kifahari aliyonayo Adebayor kwani hajawahi kupata chochote kutoka kwake licha ya nyota huyo kutesa na nyumba na magari ya kifahari.
Mwaka 2014, Adebayor aliushangaza ulimwengu wa soka baada ya kufichua mama yake alikuwa akijihusisha na vitendo vya kishirikina. Ni kipindi ambacho mchezaji huyo aliripotiwa kumfukuza mama yake kwenye nyumba aliyokuwa amemnunulia nchini Togo.
Adebayor ambaye kwa kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 30 na akilipwa Pauni 170,000 kwa wiki na Tottenham, alidai kuwa mama huyo na ndugu zake wengine walikuwa wakimroga.
Akizungumza na kituo cha televisheni cha Peace FM, nyota huyo aliitupia dongo familia yake akiiambia iache kumpiga ‘juju’. Aliongeza kuwa familia yake haipaswi kuzisogelea mali zake pindi atakapofariki.
“Wameshaanza kugawana mali zote nilizozihangaikia. Wamegawana nyumba na magari yangu,” alisema.
Adebayor aliyasema hayo baada ya dada yake aitwaye Maggie kudai kuwa mwanasoka huyo haisaidii familia yao na amekuwa hapokei simu za ndugu zake.
Kaka yake aitwaye Kola alimuunga mkono Maggie akisema: “Mama analia kila siku. Ananiambia Emmanuel (Adebayor) anamwita mchawi.”
“Mama yangu anasema sijawahi kumpa hata Dola 200 lakini nimekuwa nikiwanunulia watu magari na majumba ya kifahari,” alisema mwanasoka huyo.
“Sijui, sizungumzi na familia yangu lakini niko poa na marafiki zangu. Lakini wakitaka kuzungumza na mimi niko poa. Niko tayari kuzungumza na yeyote kwa sababu mimi ni muumini mzuri.
“Tatizo si mimi kwa sababu hawanisaidii chochote katika kufanya kazi zangu vizuri.”
Kwa upande mwingine, Adebayor amedai kuwa amebadilika kwa sasa na wala hana kinyongo na mama yake. “Mama yangu alinifanya kuwa hapa nilipo leo. Naweza kumshukuru kwa hilo.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment