News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday, 27 July 2017

OKWI ATOKA PATUPU TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA LIGI KUU UGANDA,AKOSA PESA,GARI ILA AINGIA KWENYE....


Kampala,Uganda.

NYOTA mpya wa Simba,Emmanuel Okwi jana usiku alishindwa kutamba baada ya kushindwa kutwaa tuzo yoyote kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mchezaji bora wa mwaka wa ligi kuu ya soka nchini Uganda maarufu kama Azam Uganda Premier League kwenye hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Imperial Royale iliyoko jijini Kampala.

Katika hafla hiyo mshambuliaji wa KCCA FC,Geoffrey Sserunkuma aliibuka kinara baada ya kutwaa tuzo tatu kwa mpigo ikiwemo ile ya mchezaji bora wa mwaka aliyokuwa akichuana na mshambuliaji wa Onduparaka,Mohammed Shaban pamoja na Emmnuel Okwi wa SC Villa.



Kabla ya kutangazwa mchezaji bora wa mwaka pia Sserunkuma alikuwa ametangazwa mchezaji bora chaguo la mashabiki huku pia akitajwa kwenye kikosi bora cha msimu.

Tuzo nyingine aliyotwaa Sserunkuma ni ile ya mfungaji bora wa mwaka hii ni baada ya kufunga mabao 21 msimu uliopita.

Aidha Sserunkuma alizawadiwa gari dogo la kutembelea aina ya Subaru Imprezza pamoja na kitita cha Shilingi Milioni 2 za Uganda.


Tuzo ya kocha bora imekwenda kwa Mike Mutebi wa KCCA ambaye ameitwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo.


Baadhi ya Washindi Wa Tuzo

Mchezaji Bora Wa Mwaka: Geofrey Sserunkuma (KCCA Football Club)

Mfungaji Bora: Geofrey Sserunkuma (KCCA Football Club) – 21 Mabao

Mchezaji Bora Chaguo la Mashabiki: Geoffrey Sserunkuma (KCCA Football Club)

Mchezaji Bora Chipukizi:Allan Okello (KCCA FC)

Kiungo Bora wa Mwaka:Saddam Juma (Express)

Kipa Bora Wa Mwaka: Ismail Watenga (Vipers)

Beki Bora Wa Mwaka : Halid Lwaliwa (Vipers)

Kocha Wa Makipa : Stephen Billy Kiggundu (Vipers)

Kocha Bora Wa Mwaka: Mike Mutebi (KCCA Football Club)

Mwamuzi Bora Wa Mwaka: Alex Munabi

Mashabiki Bora Wa Mwaka: Onduparaka F.C Fans

Kikosi Bora Cha Mwaka:

Ismail Watenga (G.K), Nico Wadada Wakiro, Habibu Kavuma, Halid Lwaliwa, Timothy Awanyi, Tadeo Lwanga, Muzamiru Mutyaba, Juma Saddam Ibrahim, Geofrey Sserunkuma, Shaban Muhammed,Emmanuel Okwi

Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment